UTATA KUHUSU BINADAMU WA KALLE UMEPATIVA UFUMBUZI.
Hatimaye utata uliokuwa ukiendelea duniani kwa watafiti wa mambo ya kale kuhusiana na mahali mwanadamu wa kwanza alipotokea umemalizika baada ya jopo la wataalam liloundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia ushahidi wa vinasaba kubaini kuwa binadamu huyo alitokea barani Afrika huku ikidaiwa kuwa ni Tanzania. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Japhet Hasunga ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha wadau wa mazao ya nyuki amesema kuwa utafiti huo umeshirikisha wataalamu kutoka mataifa mbalimbali duniani ambapo amesema kuwa kumalizika kwa utafiti huo utaiwezesha nchi kukua katika sekta ya utalii na kuchochea uchumi wa nchi.
No comments: